You are here: Home NEWS Local News YANGA 1- 2 DENIZLISPOR

YANGA 1- 2 DENIZLISPOR

E-mail Print PDF

VIEWED 1902 TIMES

Young Africans imepoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Denizlispor FC ya Uturuki kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika viwanja vya Selen football - Kamelya Complex pemebni kidogo ya mji wa Antalya.

Young Africans iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema zaidi lakini umaliziaji wa washambuliaji Saimon Msuva na Jerson Tegete katika dakika za 7, 15 na 24 uliikosesha mabao ya mapema.

Young Africans ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao kunako dakika ya 35, mfungaji akiwa ni Jerson Tegete akimalizia pasi safi iliyopigwa na Saimon Msuva kufuatia migongeo mizuri ya Haruna Niyonzima na Athuman Idd 'Chuji'

Young Africans ileindelea kutawala mchezo kwa kipindi chote cha kwanza na hadi timu zinakwenda mapumziko Young Africans ilikuwa mbele kwa bao 1-0

Kipindi cha pili Denizlispor FC ilifanya mabadiliko ya kikosi chake kuanzai mlinda mlango mpaka washambuliaji wake, lakini mabadiliko hayo bado hayakuweza kuisadia kwani umakii wa walinzi Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro, Kelvin Yondani na Juma Abdul ulikuwa kikwazo kwao kumfikia mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez'

Dakika ya 78 Denizlispor FC ilijipatia bao lake la kwanza, baada ya mfungaji kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni ili hali walinzi wa Young Africans na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' wakisubiri kusikia filimbi ya mamuzi kwani mfungaji kabla ya kufunga alikuwa ameunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Huku mpira ukiwa katika dakika za mwisho kabla ya kumalizika, mwamuzi wa mchezo ambaye hakuonekana kuwa makini aliwapatia wenyeji Denizlispor FC penati dakika ya 88, penati ambayo ilileta utata kutokana na mwamuzi kupishana na mshika kibendera aliyekuwa ameonyesha kuwa mshabuliaji wa Denizlispor alikuwa amemfanyia madhambi nahodha Nadir Haroub, Denizlispor FC walipiga penati hiyo na kujihesabia bao la pili na la ushindi.

Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 1- 2 Denizlispor FC.

Kocha mkuu Ernest Brandts hajapendezewa na matokeo hayo na hasa akitupa lawama zake kwa mwamuzi amabaye alishindwa kulimudu pamabano hilo ambapo katika kipindi cha pili alitoa maamuzi ya utatanishi yaliyopelekea timu yake kupoteza mchezo huo.

Timu yangu imecheza vizuri, nadhani wote tulikuwa mashuhuda jinsi vijana walivyocheza soka safi la kuvutia lililowashangaza baadhi ya wapenzi wa soka waliokuwa wamefika kutazama mchezo huo, naamini timu yangu kwa sasa iko vizuri na wachezaji wanaonekena kuelewa vizuri mafundisho yangu alisema 'Brandts'

Young Africans kesho itaendelea na mazoezi asubuhi katika viwanja vya Hoteli ya Fame Residence football .

Young Africans: Ally Mustafa 'Barthez', Juma Abdul, Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani/Mbuyu Twite, Athumani Idd 'Chuji, Saimon Msuva/Oscar Joshua, Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Didier Kavumbagu,Jerson Tegete/Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima

Last Updated ( Tuesday, 08 January 2013 19:55 )  

OUR SPONSORS

  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Young Africans kuivaa Black Leopard ya Afrika Kusini http://t.co/O5qJvtLG
yanga1935: Yanga yawasili Dar salama http://t.co/F8W53VAa
yanga1935: Yanga kutua Dar kesho alfajiri http://t.co/vdElnHqN
yanga1935: Yanga yamaliza mazoezi yake leo kwa kufanya mazoezi ya Gym http://t.co/FPbskpHa
yanga1935: Yanga yapoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Emmen FC ya Uholanzi, http://t.co/hmfEJOx9
yanga1935: International Friendly Match today: Young Africans Vs Emmen FC Kick-off: 15:00hrs (Turkey) 16:00hrs EAT Venue: Adora Football
yanga1935: Yanga kumaliza na Emmen FC kesho http://t.co/cPoDOREf
yanga1935: Yanga yaendelea kujifua Uturuki http://t.co/l98kqQDj
yanga1935: Yanga 1 - 2 Denizlispor http://t.co/L38pzkUL
yanga1935: Mpira umemalazika, Young Africans 1 - 2 Denizlispor FC Tegete dkk 35 Denizlispor dkk 78,86
yanga1935: Heres Young Africans line-up to face Denizlispor# Barthez,Juma,Kabange,Nadir,Kelvin,Chuji,Msuva,Nurdin,Didier,Kiiza & Niyonzima
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday179
mod_vvisit_counterYesterday2310
mod_vvisit_counterThis week2489
mod_vvisit_counterLast week20239
mod_vvisit_counterThis month42644
mod_vvisit_counterLast month36036
mod_vvisit_counterAll days280876

We have: 8 guests, 1 bots online
Your IP: 207.241.237.238
Mozilla 5.0, 
Today: Jan 16, 2013