You are here: Home NEWS Local News YANGA YAPONGEZWA BUNGENI

YANGA YAPONGEZWA BUNGENI

E-mail Print PDF

2012-08-06     13:37:20   VIEWED 1273 TIMES

Mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mshariki na kati kombe la Kagame, timu ya Young Africans Sports Club leo imepongezwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano Tanzania kwa kufanikiwa kutwaa Ubingwa huo.

Akiongea katika Ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge la Jahmuri ya Muungano wa Tanzania mh, Anna Makinda alisema anawapongeza wachezaji na viongozi wake wote, kwa kuliletea Taifa ubingwa huo ambao timu 11 kutoka nchi wanachama zilishiriki.

Mh Makinda alisema anafuraha siku ya leo kwa kuwa Bunge limetembelewa na wageni wengi, wakiwemo watu mashuhuri na wageni maalumu timu ya Young Africans Sports Club.

Spika alianza kwa kuwatambulisha Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Young Africans wakiongozwa na mama mlezi wa klabu hiyo, Mama Karume, Francis Kifukwe kisha akawatambulisha Mwenyekiti mpya wa Young Africans Yusuph Manji na makamu mwenyekiti Clement Sanga.

Baada ya hapo ilifuata zamu ya wachezaji na viongozi wakiwa na wazee wa klabu hyo, makofi mengi mfululizo zaidi ya dakika moja yalipigwa kwenye meza baada ya Nahodha Nadir Haroub Cannavaro kusimama na kuonyesha Kombe kwa watu wote na wabunge waliokuwepo ndani ya bunge.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na baadhi ya wabunge na mawaziri baada ya utambulisho wa Young Africans ndani ya bunge, walitoka nje kwa pamoja na kupiga picha na wachezaji na viongozi wa yanga wakiwa na kombe hilo la Kagame. 

Baada ya utambulisho, wabunge wanachama wa Young Africans waliwaalika  wageni wao wote kupata kifungua kinywa katika mgahawa wa bunge.

Wabunge wanachama wa Young Africans waliandaa kikao cha mda mfupi ndani ya ukumbe wa bunge la zamani (Msekwa Hall) ambapo wabunge, viongozi na wachezaji waliweza kufahamiana kwa undani zaidi.

Mwenyekiti Yusph Manji alifungua rasmi tawi jipya katika eneo la Bunge ambapo mwenyekiti wa Yanga tawi la bungeni ni mh. Misanga, katibu mkuu wake akiwa ni Mh Godfrey Zambi, mweka hazina mh.Martha Mlata huku Grace Kiwelu, Mwigulu Nchemba, Faki Makame, Halima Mdee, na wengineo wakitajwa kama wajumbe katika uongozi huo.

Mh Captain George Mkuchika ambaye jana aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamin wa klabu, pia ndio aliyeteuliwa kuwa mlezi wa tawi la Young Africans bungeni.

Dua za kubariki tawi hilo zilisomwa kwa pande zote mbili za dini kisha wabunge na viongozi kupiga picha za pamoja, ambapo pia jioni ya leo wabunge wameaanda futari kwa ajili ya wageni hao.

Timu inatarajiwa kureje jijini Dar kesho kuendelea na maaandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa kuanza septembe mosi.

 

Last Updated ( Monday, 06 August 2012 17:09 )  

 

   
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Green and yellow colours were dominant from the early hours of Saturday and it went on to be the dominant colours... http://t.co/sshr7bjgeQ
yanga1935: I posted 5 photos on Facebook in the album "CHAMP24NS" http://t.co/jw1L47m1kO
yanga1935: Sherehe za kukabidhiwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 kwa Mabingwa wapya Young Africans... http://t.co/S8GiejZjr7
yanga1935: Mpira umemalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC Kavumbagu ddk 4 Kiiza dkk 63
yanga1935: Dakika ya 89, Mpira umesimama kidogo, baada ya Nassoro Chollo kumsukuma Kavumbagu na wakati mwamuzi anamuulia kadondoka chini mwenyewe.
yanga1935: Dakika ya 85, anaingia Juma Abdul kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 2 - 0 Simba SC Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 1 - 0 Simba SC Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
yanga1935: Dakika ya 63, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili Young Africans 2 - Simba SC
yanga1935: Dakika ya 60, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: KUMRADHI: bao la Yanga limefungwa na Didier Kavumbagu na sio Hamis Kiiza kama nilivyoandika awali
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 30, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosa
yanga1935: Dakika ya 15, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 4, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la kwanza
yanga1935: Mpira ndo umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya wenyeji Simba SC Vs Young Africans
yanga1935: Heres Young Africans line-up to face Simba SC today: 1.Ally Mustapha - 1 2.Mbuyu Twite - 6 3.David Luhende - 29... http://t.co/XRMv18Y3vR
yanga1935: Vodacom Premier Leagu 2012/2013 Simba SC Vs Young Africans Kick-off 16:00hrs Venue: National Stadium #Tukutane... http://t.co/gD7xNq3rFs
yanga1935: Kikosi cha Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans leo kimefanya mazoezi yake... http://t.co/V6JQZYaJud
yanga1935: @ProsperMasau tiketi zitaanzwa kuuza kesho steers posta, u/taifa, buguruni shelly, sinza madukani, benjamin mkapa secondary, darlive
yanga1935: Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajia kufikia ukingoni siku ya jumamosi kwa kuchezwa michezo 7 katika... http://t.co/1q5ABNzjjj
yanga1935: Kikosi cha Young Africans leo kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Gombani kujiandaa na mchezo wake wa mwisho... http://t.co/xF73xqFibQ
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday711
mod_vvisit_counterYesterday4039
mod_vvisit_counterThis week711
mod_vvisit_counterLast week19559
mod_vvisit_counterThis month43055
mod_vvisit_counterLast month60138
mod_vvisit_counterAll days532085

We have: 31 guests, 2 bots online
Your IP: 23.22.252.150
 , 
Today: May 20, 2013