You are here: Home NEWS Local News BAADA YA KUTWAA KAGAME, WACHEZAJI WAPEWA MAPUMZIKO

BAADA YA KUTWAA KAGAME, WACHEZAJI WAPEWA MAPUMZIKO

E-mail Print PDF

2012-07-30    13:35:14  VIEWED 1036 TIMES

Uongozi wa klabu ya Young Africans Sports Club pamoja na benchi lake la ufundi, umewapa mapumziko ya wiki moja wachezaji wake wote kusheherekea Ubingwa wa Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame walioutwaa siku chache zilizopita.

Akiongea na tovuti ya klabu www.youngafricans.co.tz kocha mkuu wa Young Africans, Mbeligiji Tom Saintfiet amesema amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mashindano na kwa hakika kujituma kwao na kusikilliza maelekezo yake ndio kilichochangia mafanikio hayo.

Young Africans ilifanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya tano (5), ikiwa pia ni mara ya pili mfululizo baada ya kulitwaa kombe hilo mwaka 2011.

Katika mchezo wa fainali Young Africans iliifunga timu ya Azam FC mabao 2-0, shukrani kwa mabao ya Hamis Kiiza 'Diego' aliyefunga dakika ya 44 na Said Bahanunzi aliyefunga dakika ya 92 ya mchezo.

Kocha Tom Saintfiet amesema vijana wake wameanza mapumziko hayo toka siku ya jumamosi baada ya kutwaa Ubingwa na wanatakiwa wote kuwepo siku ya ijumaa tarehe 3/08/2012 asubuhi saa 3 katika mazoezi.

Mazoezi yataendelea kufanyika katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola mpaka itakapoanza ligi kuu ya Vodacom Septemba Mosi kama hakutakuwa na mabadiliko ya ratiba.

Kwa upande wa Uongozi, katibu mkuu wa Young Africans Mwesigwa Selestine amesema timu yake haitashiriki mashindano ya ABC Bank super8 kutokana na mashindano hayo kuja ghafla wakati kocha tayari alikuwa ameshatoa programu yake ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu.

Kwa maana hiyo Young Africans haitashiriki mashindano na itaendelea na programu ya mwalimu mpaka hapo msimu mpya wa ligi kuu utakapoanza Septemba mosi.

Pia Uongozi unawapongeza wapenzi, washabiki na wanachama wa Young Africans kwa moyo wao safi, kuishangilia timu yao toka mwanzo wa mashindano, kitu ambacho kiliwapa hamasa wachezaji kucheza na kujituma ili kuwapa furaha washabiki wao.

ICE CREAM NA KONI ZIMESHINDWA KUHIMILI JANGWANI, ZIMEYEYUKA NA KUWA MAJI  KABISAAA!!!

Fuata link hii kusikiliza/kutazama wimbo wa Hayati Pepe Kale aliouimba maalum kwa ajili ya kuipongeza Young Africans... http://www.youngafricans.co.tz/video/old-clips

 'YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO

 

Last Updated ( Monday, 30 July 2012 14:18 )  

 

   
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa... http://t.co/fkfqNHiwz1
yanga1935: Green and yellow colours were dominant from the early hours of Saturday and it went on to be the dominant colours... http://t.co/sshr7bjgeQ
yanga1935: I posted 5 photos on Facebook in the album "CHAMP24NS" http://t.co/jw1L47m1kO
yanga1935: Sherehe za kukabidhiwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 kwa Mabingwa wapya Young Africans... http://t.co/S8GiejZjr7
yanga1935: Mpira umemalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC Kavumbagu ddk 4 Kiiza dkk 63
yanga1935: Dakika ya 89, Mpira umesimama kidogo, baada ya Nassoro Chollo kumsukuma Kavumbagu na wakati mwamuzi anamuulia kadondoka chini mwenyewe.
yanga1935: Dakika ya 85, anaingia Juma Abdul kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 2 - 0 Simba SC Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 1 - 0 Simba SC Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
yanga1935: Dakika ya 63, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili Young Africans 2 - Simba SC
yanga1935: Dakika ya 60, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: KUMRADHI: bao la Yanga limefungwa na Didier Kavumbagu na sio Hamis Kiiza kama nilivyoandika awali
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 30, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosa
yanga1935: Dakika ya 15, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 4, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la kwanza
yanga1935: Mpira ndo umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya wenyeji Simba SC Vs Young Africans
yanga1935: Heres Young Africans line-up to face Simba SC today: 1.Ally Mustapha - 1 2.Mbuyu Twite - 6 3.David Luhende - 29... http://t.co/XRMv18Y3vR
yanga1935: Vodacom Premier Leagu 2012/2013 Simba SC Vs Young Africans Kick-off 16:00hrs Venue: National Stadium #Tukutane... http://t.co/gD7xNq3rFs
yanga1935: Kikosi cha Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans leo kimefanya mazoezi yake... http://t.co/V6JQZYaJud
yanga1935: @ProsperMasau tiketi zitaanzwa kuuza kesho steers posta, u/taifa, buguruni shelly, sinza madukani, benjamin mkapa secondary, darlive
yanga1935: Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajia kufikia ukingoni siku ya jumamosi kwa kuchezwa michezo 7 katika... http://t.co/1q5ABNzjjj
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday2575
mod_vvisit_counterYesterday7871
mod_vvisit_counterThis week10446
mod_vvisit_counterLast week19559
mod_vvisit_counterThis month52790
mod_vvisit_counterLast month60138
mod_vvisit_counterAll days541820

We have: 42 guests online
Your IP: 184.73.74.47
 , 
Today: May 21, 2013