You are here: Home NEWS Local News YANGA BINGWA KAGAME 2012, YAICHAPA AZAM 2-0

YANGA BINGWA KAGAME 2012, YAICHAPA AZAM 2-0

E-mail Print PDF

2012-07-28      21:14:28     VIEWED 1502 TIMES

Young Africans imefanikiwa kunyakua Ubingwa wa Vilabu kwa nchi za Ukanda wa Afrika Mshariki mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC kwa mabao 2 - 0, katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulioanza majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ulitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ai ya timu ya APR kutoka Rwanda na As Vita kutoka nchini DRC, ambapo As Vita illifanikiwa kuifunga APR kwa mabao 2-1 na kuwa mshindi wa tatu katika mashindao hayo,

Azam Fc iliyouanz amchezo huo kwa kasi, ilifanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Young Africans ikisaka bao la mapema, lakini umakini wa walinzi wa Young Africans ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji  John Boko na Kipre Tcheche.

Huku Azam ikiendelea kuutawala mchezo kwa dakika 30 za kipindi cha kwanza, dakika ya 32 nusura Haruna Niyonzima aipatie timu yake bao la kuongoza lakini shuti lake hafifu lilidakwa na mlinda mlango wa timu ya Azam  fc Deogratius Munsihi 'Dida'.

Young Africans ilibadilika na kuendelea kufanya mashambulizi langoni mwa timu ya Azam na katika dakika ya 44, Hamis Kiiza 'Diego' aliipatia Young Africans bao la kwanza, baada ya kuunasa mpira uliopigwa na mlinzi Aggrey Morris aiyekuwa akimrudishia golikipa wake na Kiiza kuuwahi na kuuweka kimiana na kuandika bao la kwanza.

Mpaka mpira unakwenda mapumziko Young Africans ilikuwa mbele kwa bao 1 - 0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam fc kufanya mabadiliko amabapo iliwatoa Jabir Aziz na Kipre Tcheche na nafasi zao kuchukuliwa na Haji Nuhu na Mrisho Ngasa ambao bado hawakuweza kuubadili mchezo.

Azam fc nusura ipate bao la kusawazisha kupitia kwa mmshambuliaji wake John Boko, lakini mpira wa kichwa aliopiga kuelekea langoni uliokolewa na mlinzi Stephano Mwasika amaby leo alicheza nafasi ya mlinzi wa kulia ili hali akitumia mguu wa kushoto.

Dakika ya 62, Haruna Niyonzima alikosa tena bao la wazi kufuatia kazi nzuri iiyofanywa na Said Bahanunzi ,lakini Niyonzima alipiga shuti kubwa akiwa yeye a mlinda mlango wa Azam na kupaisha juu ya lango na kuwa mpira wa kutoka.

Rashid Gumbo alioka dakika ya 73 na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Seif Kijiko, ambapo Young Africans iliendelea kuutawala mchezo kipindi chote za pili mpaka kuelekewa dakika za lala salama.

Huku washabiki , wapenz na wanachama wa Young Africans wakiianza kutoka nje wakijua tayari mpira umekwisha, Said Bahanunzi aliipatia Young Africans bao la pili kwa shuti kali kufuatia kuwatoka walinzi wa Azam na kumtungua Dida kwa shuti kali la mguu wa kushoto na kutinga nyavu za juu.

Mpaka mchezo unamalizika Young Afrians 2- 0 Azam .

Young Africans imefanikiwa kutwa Ubingwa huu kwa mara ya pili mfululizobaada ya kulichukua mwaka jana katika mchezo uliofanyika pia jijini Dar es salam na uwafunga Simba kwa bao 1- 0, bao la mshambuliaji kutoka nchini Ghana Kenneth Asamoah na ikiwa ni mara yake ya tano (5) tangu kuanzishwa kwake, 

Said Bahanunzi ameibuka kuwa mfungaji bora wa mshindao hayo, baada ya kufunga jumla ya mabao sita (6) akifuatiwa na Teddy wa As Vita mwenye mabao sita pia lakini moja likiwa ni la penati na Hamis Kiiza ameibuka wa tatu kwa kufunga mabao tano (5).

Young Africans: 1.Ally Mustafa 'Barthez', 2.Stephao Mwasika, 3.Oscar Joshua, 4.Kelvin Yondani, 5.Nadir Haroub 'Cannavaro' (c), 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Rashid Gumbo/Juma Seif 'Kijiko', 8.Haruna Niyonzima, 9.Said Bahanunzi, 10.Hamis Kiiza 'Diego, 11.David Luhende 

Azam FC: 1.Deogratius Munishi 'Dida', 2.Ibrahim Shikanda, 3.Erasto Nyoni, 4.Said Morad, 5.Aggrey Morris, 6.Jabir Aziz/Haji Nuhu, 7.Ibrahim Mwaipopo, 8.Salum Abubakar, 9.John Boko, 10.Kipre Tcheche/Mrisho Ngassa, 11.Ramadhani Chombo 'Redondo.

Last Updated ( Sunday, 29 July 2012 14:11 )  

 

   
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Droo ya makundi kwa ajli ya mashindano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati al-maarufu kama (KAGAME CUP)... http://t.co/r2esjJLwtJ
yanga1935: Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa... http://t.co/fkfqNHiwz1
yanga1935: Green and yellow colours were dominant from the early hours of Saturday and it went on to be the dominant colours... http://t.co/sshr7bjgeQ
yanga1935: I posted 5 photos on Facebook in the album "CHAMP24NS" http://t.co/jw1L47m1kO
yanga1935: Sherehe za kukabidhiwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 kwa Mabingwa wapya Young Africans... http://t.co/S8GiejZjr7
yanga1935: Mpira umemalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC Kavumbagu ddk 4 Kiiza dkk 63
yanga1935: Dakika ya 89, Mpira umesimama kidogo, baada ya Nassoro Chollo kumsukuma Kavumbagu na wakati mwamuzi anamuulia kadondoka chini mwenyewe.
yanga1935: Dakika ya 85, anaingia Juma Abdul kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 2 - 0 Simba SC Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 1 - 0 Simba SC Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
yanga1935: Dakika ya 63, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili Young Africans 2 - Simba SC
yanga1935: Dakika ya 60, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: KUMRADHI: bao la Yanga limefungwa na Didier Kavumbagu na sio Hamis Kiiza kama nilivyoandika awali
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 30, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosa
yanga1935: Dakika ya 15, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 4, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la kwanza
yanga1935: Mpira ndo umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya wenyeji Simba SC Vs Young Africans
yanga1935: Heres Young Africans line-up to face Simba SC today: 1.Ally Mustapha - 1 2.Mbuyu Twite - 6 3.David Luhende - 29... http://t.co/XRMv18Y3vR
yanga1935: Vodacom Premier Leagu 2012/2013 Simba SC Vs Young Africans Kick-off 16:00hrs Venue: National Stadium #Tukutane... http://t.co/gD7xNq3rFs
yanga1935: Kikosi cha Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans leo kimefanya mazoezi yake... http://t.co/V6JQZYaJud
yanga1935: @ProsperMasau tiketi zitaanzwa kuuza kesho steers posta, u/taifa, buguruni shelly, sinza madukani, benjamin mkapa secondary, darlive
yanga1935: Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajia kufikia ukingoni siku ya jumamosi kwa kuchezwa michezo 7 katika... http://t.co/1q5ABNzjjj
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday1029
mod_vvisit_counterYesterday3273
mod_vvisit_counterThis week16642
mod_vvisit_counterLast week19559
mod_vvisit_counterThis month58986
mod_vvisit_counterLast month60138
mod_vvisit_counterAll days548016

We have: 38 guests, 3 bots online
Your IP: 54.235.20.17
 , 
Today: May 23, 2013