You are here: Home NEWS Local News YANGA, AZAM ZAINGIZA MIL 72/-

YANGA, AZAM ZAINGIZA MIL 72/-

E-mail Print PDF
2012-03-13       13:08:49       VIEWED 288 TIMES 
YANGA, AZAM ZAINGIZA MIL 72/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam lililochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 72,731,000.
 
Jumla ya watazamaji 19,339 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh. 15,000.
 
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,303,932.20 kila timu ilipata sh. 14,726,592.20, uwanja sh. 4,908,864.07.
 
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,963,545.63, TFF sh. 4,908,864.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,454,432.03, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 490,886.41 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,908,864.07.
 
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. waamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, tiketi sh. 3,540,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
 
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata tena sh. 1,353,730 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 1,160,340.
 
Wakati huo huo kesho timu ya Yanga itashuka dimbani kucheza na timu ya African Lyon katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Vodacom nchini. Yanga itashuka dimbani kusaka pointi 3 muhimu ili kuweza kuendelea kusogea katika nafasi nzuri ya kutetea Ubingwa wake.
Wapenzi washabiki na wanachama mnaombwa kujitokeza kwa wingi kuendelea kuishangilia timu yenu. 
 
Last Updated ( Tuesday, 13 March 2012 14:45 )  

 

   
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: I posted 5 photos on Facebook in the album "CHAMP24NS" http://t.co/jw1L47m1kO
yanga1935: Sherehe za kukabidhiwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 kwa Mabingwa wapya Young Africans... http://t.co/S8GiejZjr7
yanga1935: Mpira umemalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC Kavumbagu ddk 4 Kiiza dkk 63
yanga1935: Dakika ya 89, Mpira umesimama kidogo, baada ya Nassoro Chollo kumsukuma Kavumbagu na wakati mwamuzi anamuulia kadondoka chini mwenyewe.
yanga1935: Dakika ya 85, anaingia Juma Abdul kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 2 - 0 Simba SC Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 1 - 0 Simba SC Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
yanga1935: Dakika ya 63, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili Young Africans 2 - Simba SC
yanga1935: Dakika ya 60, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: KUMRADHI: bao la Yanga limefungwa na Didier Kavumbagu na sio Hamis Kiiza kama nilivyoandika awali
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 30, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosa
yanga1935: Dakika ya 15, Young Africans 1 - 0 Simba SC
yanga1935: Dakika ya 4, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la kwanza
yanga1935: Mpira ndo umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya wenyeji Simba SC Vs Young Africans
yanga1935: Heres Young Africans line-up to face Simba SC today: 1.Ally Mustapha - 1 2.Mbuyu Twite - 6 3.David Luhende - 29... http://t.co/XRMv18Y3vR
yanga1935: Vodacom Premier Leagu 2012/2013 Simba SC Vs Young Africans Kick-off 16:00hrs Venue: National Stadium #Tukutane... http://t.co/gD7xNq3rFs
yanga1935: Kikosi cha Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans leo kimefanya mazoezi yake... http://t.co/V6JQZYaJud
yanga1935: @ProsperMasau tiketi zitaanzwa kuuza kesho steers posta, u/taifa, buguruni shelly, sinza madukani, benjamin mkapa secondary, darlive
yanga1935: Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajia kufikia ukingoni siku ya jumamosi kwa kuchezwa michezo 7 katika... http://t.co/1q5ABNzjjj
yanga1935: Kikosi cha Young Africans leo kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Gombani kujiandaa na mchezo wake wa mwisho... http://t.co/xF73xqFibQ
yanga1935: Somewhere in Pemba Island http://t.co/Q8sX0Dgxx7
yanga1935: Young Africans Players in Camp at Pemba Island @Yanga1935 http://t.co/LfnUq2WFth
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday1132
mod_vvisit_counterYesterday4599
mod_vvisit_counterThis week16652
mod_vvisit_counterLast week14708
mod_vvisit_counterThis month39437
mod_vvisit_counterLast month60138
mod_vvisit_counterAll days528467

We have: 54 guests, 4 bots online
Your IP: 107.22.127.92
 , 
Today: May 19, 2013