2012-03-07 11:07:28 VIEWED 453 TIMES
Kikosi cha Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Young Africans Sports Club kimeendelea na mazoezi katika viwanja wa vya shule ya Sekondari Loyola na shule ya IST kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya timu ya Azam FC siku uya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo mwishoni mwa wiki ilicheza na Zamalek ya Misri katika mchezo wa marudiano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika na kufungwa bao 1 - 0, ilirejea jumatatu asubuhi ambapo wachezaji walipewa mapumziko mpka siku ya jumanne walipoanza mazoezi ya pamoja.
Baada ya kutolewa katika mashindano ya kimataifa na Zamalek kwa jumla ya mabao 2-1, Young Africans inaelekeza nguvu zake katika kutetea Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom jumamosi kwa kucheza na Azam FC inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini.
Kocha Mkuu Kostadian Papic amesema wachezaji wake walicheza vizuri katika mchezo wao jijini Cairo licha ya kufungwa bao 1- 0 na wenyeji wao, pia aliongeza kutolewa kwa Chuji kwa kadi nyekundu kulichangia timu kukosa ushindi kutokana na kucheza pungufu kwa mda mrefu huku akilalamikia hali ya hewa ya baridi iliyowasumbua wachezaji wake.
Katika kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo wa jumamosi Young Africans inaingia kambini leo jioni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi dhidi ya wana lamba lamba.
Wachezaji wanaofanya mazoezi ni pamoja na:
Walinda Milango; Shaban Hassan Kado, Said Mohamed,
Walinzi wa Pemebeni; Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Abuu Ubwa, Stephano Mwasika,
Walinzi wa Kati; Chacha Marwa, Ibrahim Job, Bakari Mbega, Nadir Haroub Cannavaro, Zuberi Ubwa,
Viungo wa Ulinzi; Juma Seif Kijiko, Godfrey Bonny,Athuman Iddy Chuji
Viungo Washambuliaji; Haruna Niyonzima, Nurdin Bakari, Rashid Gumbo, Athuman iddy Chuji
Viungo wa Pembeni; Omega Seme, Shamte Ally, Idrisa Rashid, Kiggi Makassy,
Washambuliaji; Kenneth Asamoah, Pius Kisambale, Davies Mwape, Jeryson Tegete
Aidha Benjamin Berko aliyekuwa majeruhi kwa mda mrefu, tayari amepona na amaenza mazoezi mepesi ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya ufukweni.
Salum Telela anaendelea na matibabu ya kifundo cha mguu
Hamis Kiiza anaendelea na matibabu ya mbavu zilizomsababisha asicheze mechi ya Cairo















