You are here: Home NEWS Local News YANGA, ZAMALEK ZATOKA SARE

YANGA, ZAMALEK ZATOKA SARE

E-mail Print PDF

2012-02-18       22:03:49       VIEWED 277 TIMES 

Timu ya Young Africans imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Zamalek FC kutoka nchini Misri, katika mchezo wa kwanza wa Klabu Bingwa Afrika uliochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wapenzi na washabiki wengi wa soka nchini Tanzania.

Young Africans itabidi ijilaumu kwa kukosa mabao mengi ya wazi kupitia washambuliaji wake Davies mwape, Kenneth Asamoah na Omega Seme amabo hawakua makini kataika umaliziaji.

Young Africans ilianza mchezo kwa kasi na katika dakika ya 15 ya mchezo, mshambuliaji Kenneth Asamoah alishindwa kuipatia timu yake bao la kuongoza baada ya kubaki yeye na mlinda mlango wa Zamalek FC Abdel Wahed el Sayed na kupiga shuti hafifu lililodakwa na mlinda mlango huo.

Huku wakionekana wenye ari ya ushindi na kutaka kupata bao la mapema, Young Afrcans walikosa tena bao la wazi dakika ya 18 ya mchezo kupitia kwa Hamis Kiiza na Omega Seme alishindwa kuifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 22, mara baada ya kupata safi kutoka kwa Stephano Mwasika na Omega kupiga shuti hafifu.

Razack Omotyossi alipata nafasi nzuri ya kuweza kufunga bao katika dakika ya 27 akiwa amebaki yeye na mlinda mlango wa Young Africans, lakini umakini wa mlinda mlango Shaban Hassan Kado uliweza kuzuia shambulizi hilo. Zamalek walionekana kuzidiwa sehemu ya katikati na viungo wa Young Africans hali iliyopelekea wafanye mabadiliko dakika ya 35 ya mchezo, mabadiliko ambayo hayakuisaidia timu hiyo.

Hamis Kiiza Diego aliipatia Young Africans bao la kwanza mnamo dakika ya 36, mara baada kumzidi ujanja mlinzi wa Zamalek na kupiga shuti lililomzidi mlinda mlango Abdel na kuingia wavuni na kuihesabia timu yake bao la kwanza. Mara baada ya kuingia kwa bao hilo Young Africans waliamka na kufanya mashabulizi katika ya 38 ya mchezo Davies Mwape alishindwa kuipatia timu yake bao la pili baada kushindwa kumalizia pasi ya Hamis Kiiza.

Dakika ya 45 Kenneth Asamnoah alishindwa kuipatia timu yake bao la pili baada ya kupiga shuti dhaifu liliodakwa na mlinda mlango wa Zamalek. Mpaka mapumziko Young Africans 1 - 0 Zamalek FC

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa tahadhari, huku Zamalek wakicheza kwa kujilinda wasifungwe bao jingine na Young Africans wakisaka bao la pili. Dakika ya 58 Zamalek walifanya mabadiliko amabpo Amry Zaki aliingia kuchukua nafasi ya Isalam Awad.

Mabadiliko hayo hayakuwa na msaada wowote kwa Zamalek kwani dakika ya 65 ilibidi wafanye mabadiliko mengine ya tatu. Young Africans ilifanya mabadilko dakika ya 73 ambapo Shamte Ally aliingia kuchukua nafasi ya  Davies Mwape.

Amry Zaki aliipatia Zamalek bao la kusawazisha dakika ya 75 mara baada ya uzembe wa beki wa kulia kumuacha mfungaji akizania amezidi, na mfungaji huyo kumfikia mlinda mlango Shaban Hassan Kado na kufunga bao hilo.

Kenneth Asamoah atalaumiwa na washabikiwengi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo kwani katika dakika ya 78 tena alikosa bao la wazi akiwa na yeye na mlinda mlango wa Zamalek, ambapo Asamoah alimpiga chenga mlinda mlango huyo na kupiga shuti hafifu lililozuiliwa na mlinzi wa Zamalek.

Oscar Joshua aliingia kuchukua nafasi ya Stepano Mwasika dakika ya 81,mabadiliko ambayo hayakusaidia kubadilisha matokeo kwa upande wowote wa mchezo kwani mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho ya mchezo Young Africans 1 - 1 Zamalek FC.

Kimchezo Young Africans ilicheza mchezo mzuri tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho wa mchezo huo, tatizo kubwa lilionekana ni umakini kwa washabuliaji wake kuwa na papara wanapokuwa langoni mwa timu pinzani, kitu kilichowakosesha mabao zaidi ya matano ya wazi. Mlinda mlango na walinzi walifanya kazi yao ipaswvyo, huku Haruna Niyonzima na Juma Seif Kijiko wakingaa katika eneo la dimba la katikati.

Young Africans itarudiana na Zamalek wiki mbili zijazo mwezi Machi kati ya taehe 2,3 au 4

Young Africans: 1.Shaban Kado, 2.Shadrack Nsajigwa, 3,Stepahano Mwasika/Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub Canavaro, 5.Athuman Iddy Chuji, 6.Juma Seif Kijiko, 7.Omega Seme, 8.Haruna Niyonzima, 9.Davies Mwape/ShamteAlly , 10.Kenneth Asamoah, 11.Hamis Kiiza

Zamalek FC: 1.Abdelwahed El-Sayed,2.Mohamed Abdel-Shafy, 3.Hani Saed, 4.Alexix Enam, 5.Nour El Sayed, 6.Ahmed Samir/Amr Zaki, 7.Sabry Raheel/Hazem Mohamed, 8.Mahmoud Fathallah, 9.Islam Awad/Said Mohamed, 10.Razack Omotoyyosi, 11. Ahmed Hassan

Last Updated ( Sunday, 19 February 2012 14:38 )  

OUR SPONSORS

   
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday14
mod_vvisit_counterYesterday175
mod_vvisit_counterThis week1346
mod_vvisit_counterLast week1074
mod_vvisit_counterThis month3458
mod_vvisit_counterLast month5230
mod_vvisit_counterAll days29457

We have: 1 guests, 1 bots online
Your IP: 38.107.179.241
 , 
Today: May 21, 2012