2012-02-17 14:12:47 VIEWED 385 TIMES

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Kostadian Papic amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wake dhidi ya Zamalek ya Misri ambayo imewasili jijini Dar es Salaam leo alfajiri tayari kwa mchezo wake hapo kesho siku ya Jumamosi wakati itakapokutana na Yanga wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika.
Papic amesema hayo mbele ya waandishi wa Habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF ambapo kocha huyo aliambatana na Kapteni wa Yanga Shedrack Nsajigwa wakati wa Mkutano wa pamoja na kocha Msaidizi wa Zamaleck Ossama Nabih ambaye alifuatana na nahodha wake Abdel Wahed el Sayed.
Akizungumzia hali za wachezaji wake Papic amesema wachezaji watano huenda hawatacheza kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, Kocha aliwataja wachezaji hao ambao ni Godfrey Bonny,Yaw Berko,Rashid Gumbo,Nurdine Bakari pamoja na Salum Telela.
Kuhusu pambano lenyewe kocha amesema ingawa timu ya Zamalek inauzoefu na michuano hiyo anaamini kuwa Kikosi cha Yanga kitafanya vizuri katika pambano hilo. Kwa upande wake kocha msaidizi wa timu ya Zamalek Ossama nabih amesema wanaifahamu vyema timu ya Yanga kuwa ni timu kubwa lakini timu yake itaonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo na kutoa burudani kwa mashabiki watakaoshudia pambano hilo.
Pamoja na kukataa kutoa majina ya kikosi cha timu ya Zamalek waliowasili jijini Dar Salaam Utafiti uliofanywa na mtandao wa Yanga www.youngafricans.co.tz umebaini wachezaji waliowasili. Miongoni mwa wachezaji hao ni Nahodha Abdel Wahed el-Sayed, Ahmed Samir, Ahmed Gaafar, Ibrahim Mohamed, Mahmood Fathalaa, Abdel Shafy, Nour El Syaed, Saeed Kota, Alla Aly, Hany Said, Mohamed Genesh, Sabry Rahil, Ahmed Tawfik, Razack Omotoyossi, Alexix Mendono, Amr Zaki, Hazem Emam, Islam Awad, Amir Gaber, Ahmed Menherawy, na Mostafa El Sayed.
Uongozi wa klabu wa Yanga unawaomba wapenzi, washabiki na wanachama kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao uwanjani.
Nyimbo 3 zimepitishwa kutumika katika ushangiliaji wa Yanga, fuata link hapa chini uweze kudownload na kuzijua nyimbo hizo za ushangiliaji:
1.HAROON TEAM http://hu.lk/b01fkswswuu4
2.NASH SOCCER http://hu.lk/4tx2d44kndip
3.MR CHUMVI http://hu.lk/fuqzs33l9nll















