2012-02-15 15:42:15 VIEWED 278 TIMES

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania pambano la Yanga na Zamalek limeingia katika historia mpya kufuatia tiketi za mchezo huo kuwa za kisasa ambazo tayari zimekwisha tua nchini. Kindamba amesema tiketi hizo zitasaidia kufahamu idadi ya watu watakaoingia uwanjani hapo kabla ya pambano hilo kuanza.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa Kampuni ya Prime Times Promotion Balozi Kindamba, amesema tiketi hizo ni za kisasa ambazo ni vigumu mtu kutengeneza za bandia.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika, utaratibu utakaotumika ni wa kisasa kabisa, kila mtu atakaa kwenye kti chake bila bughuza yoyote, ulinzi utakua wa uhakika kwa usalama wa wachezaji, washabiki watakaojitokeza uwanjani kushuhudia mchezo huo alisema Kindamba.
Viingilio vya pambano la hilo kati ya Yanga na Zamalek ya Misri litakalochezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam vimetangazwa
VIP A Tshs 50,000/=,
VIP B Tshs 30,000/=
VIP C Tshs 10,000/=
Rangi ya machugwa Tshs 7,000/=
Rangi ya Bluu Tshs 5,000/=
Rangi ya Kijani Tshs 3,000/=
Naye Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Boniface Wambura amesema tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Alhamisi katika vituo kumi vilivyochaguliwa.
Vituo ambavyo vitauza tiketi za mchezo huo kuanzia kesho alhamis ni:
Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa,
Steers Posta mpya,
Big Bon Kariakoo,
Ubungo Oil Com,
VETA Oil Com,
Uwanja wa Taifa
Oil Com Mbagala,
Oil Com Mtoni kwa Aziz Ally,
Oil Com Tabata,
Majumba Sita Banana) na
Mwembe Yanga Tandika.
Wakati huo huo, kikosi cha timu ya Yanga kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Zamalek siku ya jumamosi, wachezaji wote wapo kwenye ari ya mchezo huo.
Kocha mkuu Kostadin Papic amesema wachezaji wake wanaonekana kuelewa na kuyashika maelekezo yake hivyo ana amini siku ya jumamosi watacheza soka safi na kuibuka na ushindi.
Katika mchezo huo wa jumamosi Yanga itawakosa wachezaji wawili ambao ni majeruhi,
Nurdin Bakari (kidole)
Salkum Telela (Enka)















