2012-02-12 21:37:37 VIEWED 188 TIMES

Timu ya Young Africans Sports Club imesheherekea miaka 77 kwa ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom . Mchezo huo wakuvitia ulifanyika katika Uwanja wa Taifa jjijini Dar es Salaam na kushuhudia timu zote zikionyesha kandanda safi na la kuvutia lakini mpaka mwisho wa mchezo huo Young Africans imefanikiwa kurudi kileleni na kushika usukani wa ligi kuu ya Vodacom nchini Tanzania Bara.
Young Africans iliyokuwa inasheherekea miaka 77 tangu kuasisiwa kwake, ilianza mchezo kwa kasi na kufanya mashambulizi mfululizo toka sekunde ya kwanza ya mchezo, katika dakika ya 22 ya mchezo, mshambuliaji Davies Mwape alishindwa kuipatia timu yake bao la kuongoza baada ya kumpiga chenga mlinda mlando wa Ruvu Shooting Benjamin Haule na kushindwa kuukwamisha wavuni mpira uliotoka sentimeta chache langoni.
Dakika ya 30 Young Africans ilipata penati iliyotolewa na mwamuzi wa mchezo mara baada ya mlinzi wa Ruvu Shooting Shaban Sunze kumchezea madhambi mshambuliaji Davies Mwape, Hamis Kiiza alikwenda kuipiga penati hiyo na kukosa, ambapo mlinda mlango Benjamin Haule aliupangua na kuwa na kona.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika mpira Young Africans 1 - 0 Ruvu Shooting. Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo Shamte Ally aliingia kuchukua nafasi ya Omega Seme.
Mabadiliko hayo yalileta furaha kwa wapenzi na washabiki wa Young Africans katika dakika ya 46, baada ya Davies Mwape kuifungia timu yake bao la kwanza kwa shuti kali liligonga mwamba wa juu na kuingia moja kwa moja wavuni na kuhesabau bao la kwanza la Young Africans.
Dakika ya 53 Juma Seif Kijko alikosa bao la wazi baada ya kupiga shuti hafifu, Ruvu Shooting ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Seif Abdallah, Abrahamn Abrahaman waliochukua nafasi za Rapahael Kyala na Kassim Linde, mabadiliko hayakuzaa matunda yoyote.
Kenneth Asamoah alikosa mabao ya wa wazi dakika ya 68, 76 akiwa na yeye na mlinda mlango Benjamin Haule baada ya kupiga mashuti hafifuyaliyokolewa na mlinda mlango huyo.
Dakika ya 80, 86 Ruvu Shooting ilifanya mashambuliz ya kushitukiza langoni mwa lango la Young Africans lakini umakini wa mlinda mlango wa Young Africans Shaban Hassan 'Kado' ulizima ndoto za kupata bao la kusawazisha.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 1- 0 Ruvu Shooting, matokeo hayo yanaipelekea Young Africans kurudi kileleni na kukamata usukani wa ligi kuu ya Vodacom, huku pia ikishehereka ushindi huo na maadhimisho ya 77 tangu kuasisiwa kwake.
Young Africans: 1.Kado, 2.Job/Chacha (86), 3,Mwasika, 4.Canavaro (C), 5.Chuji, 6.Kijiko, 7.Omega/Shamte(45), 8.Niyonzima, 9.Mwape, 10.Asamoah/Tegete(77), 11.Kiiza
Ruvu Shooting: 1.Haule(C), 2.Pius, 3.Ngalema, 4.Nyambiso, 5.Sunze, 6.Japhari, 7.Kitala, 8.Dilunga, 9.Linde/Seif(56), 10.Kijuso/A.Juma(70), 11.Kyalla/Abrahman(56)
Awali kabla ya mchezo huo, kulikuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Young Africans (Veteran) na Clouds FM Media amabapo mpaka mwisho wa mchezo Young Veteran iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Young Africans inaendeela kujiandaa na mchezo wake wa Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya timu ya Zamalek FC ya Misri , mchezo utafanyika siku ya jumamosi tarehe 18/02/2012















