VIEWED 1435 TIMES

Aliyekuwa Dereva wa Bus kubwa la wachezaji wa klabu ya Young Africans Bw Maulid Kiula anatarajiwa kuzikwa leo mchana katika eneo la Kibaha, baada ya kuagwa asubuhi na wachezaji, viongozi pamoja na wanachama katika Hospital ya Amana Ilala jijini Dar es salaam.
Kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo, wasaidizi wake pamoja na wachezaji walifika hospitali ya Amana mara tu baada ya kumaliza mazoezi ya asubuhi na kutoa heshima za mwisho kabla ya safari kuelekea Kibaha kwenye mazishi.
Marehemu Maulid Kiula alikuwa mfayakazi wa klabu ya Young Africans katika idara ya usafirishaji, na katika kipindi cha uhai wake alikuwa akiendesha Bus Kubwa la Wachezaji (Yutong) kwenye shughuli mbali mbali ikiwa ni mazoezini na kwenye safari za mikoani.
Akiwa Yanga marehemu Kiula alikuwa rafiki wa wachezaji, viongozi na wanachama kwa ujumla hali iliyompelekea kuifanya kazi yake bila usumbufu wowote.
Uongozi wa klabu ya Young Africans unatoa pole kwa ndugu, jamaa na famili ya marehmu kwa msiba huu mkubwa uliotokea.
Inna Iillah Wainna Illah Rajiun.







