VIEWED 2165 TIMES

Young Africans Sports Club yenye makao makuu yake mitaa ya Twiga/Jangwani kesho itashuka katika dimba la Uwaja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakaribisha wauza maji/ramba ramba timu ya Azam FC ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2013/2014.
Kikosi cha Young Africans ambacho kimeweka kambi mjini Bagamoyo kmeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo ambao umebeba taswira ya mbio za Ubingwa kwani timu zote mbili Azam FC ikiwa inaongoza kwa tofauti ya pointi 4 huku ikiwa na mchezo mmoja mbele zaidi.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der Pluijm amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi katika kambi, mchezaji pekee atakayeukosa mchezo huo ni Deo Munish "Dida" ambaye alipata majeraha ya kuumia mkono mwishoni mwa wiki na kwa sasa anaendelea na matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa timu Dr Suphian Juma.
Kuhusu wachezaji Haruna Niyonzima na Mrisho Ngasa walioukosa mchezo wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na kuwa wagonjwa kwa sasa wako fit na wameshaungana na timu tangu siku ya jumapili tayari kwa maandalizi pamoja na wachezaji wengine kuelekea kwenye mechi hiyo jumatano.
Benchi la Ufundi la Young Africans limesema vijana wao wapo vizuri kwa mchezo wa kesho, morali, kiafya na dhamira ya kupata ushindi ni kubwa hivyo wanaamini kwa jinsi walivyowaandaa vijana watafanya vizuri na kupata ushindi.
Mchezo huo wa kesho unatarajiwa kuanza majira ya saa 10:30 kwa sa za Afrika Mashariki.







