";} /*B6D1B1EE*/ ?>
You are here: Home NEWS Local News YANGA YAWASILI SALAMA CAIRO

YANGA YAWASILI SALAMA CAIRO

E-mail Print PDF

VIEWED 5574 TIMES

Kikosi cha Young Africans kimewasili salama jijni Cairo alfajiri ya leo kwa shirika la ndege la Egypt Air ikiwa na msafara wa watu 31 wakiweo viongozi pamoja na wachezaji na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Bw Mohamed Hamza kisha kuondoka kwa msafara Uwanja wa Ndege kuelekea hoteli ya Nile Paradise Inn.

Viongozi wa Al Ahly walifika Uwanja wa Ndege wa Cairo wakiwa wamshaanda usafiri wa kukipokea kikosi hicho lakini uongozi wa Yanga uliokuwa umeshatangulia nchini Misri kwa kushirikiana na Ubalozi ulikuwa umeshandaa usafiri mwingine hivyo wachezaji na viongozi walipotoka ndani moja kwa moja walikwenda kupanda bus maalumu waliondaliwa na kuwaacha Al Ahly wakishangaa.

Mapema alfajiri katika Uwanja wa Ndege wa Cairo vyombo vya habari jijini hapa vilijotokeza kuishuhudia Young Africans huku wakitaka kuwajua wachezaji walokuja nchini Misri na kuomba kujua hoteli ambayo timu itafikia kufuatia kuikataa hoteli walyokua wameiandaa wenyeji ya Baron iliyopo eneo la new Cairo.

Baadhi wa waandishi waliapata nafasi ya kuongea na kocha mkuu wa Young Africans Hans Van Der Pluijm uwanja wa Ndege wakitaka kujua kikosi kimeajiandaaje kwa mchezo huo wa jumapili ambapo kocha Hans aliwaambia Young Africans imejiandaa vyema kuelekea mchezo na wapo tayari kucheza sehemu yoyote siku ya jumapili.

Mara baada ya majibu hayo msafara wa Young Africans ulielekea Hoteli ya Nile Paradise Inn kwa kuongozana na Balozi Hamza pamoja na wasaidizi wake amapo mara baada ya kuwasili hotelini Balozi aliwapa pole vijana kwa uchovu wa safari kisha kuwaambia wana jukumu kubwa la kuipeperusha vizuri bendera ya nchi katika mchezo wa jumapili na wao kwa kushirikiana na Serikali wapo tayari kutoa msaada wowote utakaoihitajika ili mradi kuisadia timu iweze kufanya vizuri.

Kuhusu uwanja wa mchezo mpaka jioni ya leo bado ni kizungumkuti kufuatia Al Ahly kushindwa kutoa taarifa rasmi juu ya ni sehemu gani mchezo utakapofanyika, kwani mara baada ya kikao na viongozi wa Yanga leo asubuhi akiwemo Makamu Mwenyekiti Clement Sanga, Afisa Habari Baraka Kizuguto, Mjumbe wa kamati ya mashindano Beda Tindwa, Mkuu wa usalama ubalozi wa Tanzania Col Othman na kuahidi kutoa majibu baada ya masaa matatu lakini mpaka giza linaingia bado hawajaweza kutoa majibu kamili.

Pamoja na mkanganyiko huo wa ni uwanja gani mchezo utakapofanyika Uongozi wa Yanga umejiandaa kwa lolote na upo tayari kucheza mchezo huo wa jumapili eneo lolote mamlaka husika ya usalama itakapoamuru ufanyike.

Majira ya saa 1 jioni kwa saa za huku kikosi kimefanya mazoezi ya kwanza katika Uwanja uliopo hoteli ya Nile kujaindaa na mchezo huo wa siku jumapili.

Last Updated ( Friday, 07 March 2014 16:47 )  

  • FACEBOOK

  • TWITTER