VIEWED 4065 TIMES

Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Young Africans imeingia kambini katika hotel ya Laico Ledger iliyopo eneo la Bahari Bahari Beach Kunduchi kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Al Ahly kutoka nchini Misri mchezo utakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Young Africans chenye wachezai 25 pamoja na benchi la Ufundi kilianza mazoezi jana jioni katika Uwanja wa Kaunda Makao Makuu ya Klabu na leo asubuhi imeendelea kujinoa katika Uwanja wa Boko Beach.
Kocha Mkuu wa Young Africans Mholanzi Hans Van der Pluijm amesema anashukuru vijana wake wote wapo katika hali nzuri, jana wamefanya mazoezi pamoja na leo asubuhi mpaka sasa hakuna mchezaji majeruhi kuelekea mchezo wa jumamosi.
Akiongelea mchezo wa jumamosi Hans amesema wanatambua mchezo dhidi ya Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi siku ya jumamosi utakua ni mgumu, kwani Al Ahly wana uzoefu na michezo ya kimataifa lakini na sisi lengo letu ni kufanya mapinduzi kwa kushinda mchezo wetu wa nyumbani.
Hans amesema hakuna kinachoshindikana katika mpira wa miguu, nimewahi kucheza nao nilikiwa Ghana na timu ya Berekum Chelsea katika hatua ya makundi ya robo fainali, hivyo nawajua vizuri jinsi wanavyocheza na kocha Mkwasa alipata fursa ya kuwaona wiki ilyopita tunaamin mambo yatakua mazuri.
"Kikubwa tunakiandaa kikosi chatu kiwe tayari kwa mchezo, kiakili, morali, umoja na nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya Uwanja" alisema Hans.
Wakati huo huo Timu ya Al Ahly inatarajiwa kuwasili kesho alfajiri saa 12 kasorobo kwa Shirika la Ndege la Misri Egypt Air na moja moja kwa moja watakifikia katika Hotel ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta ambapo ndio itakua kambi yao kuelekea mchezo wa jumamosi.
Balozi msaidizi wa Misri nchini Tanzania Balozi Ibrahim ambaye amekuwa akishirikiana muda wote na viongozi wa Young Africans amesema timu ya Al Ahly inatarajiwa kuwasili na msafara wa watu 35 wakiwemo wachezaji 22, bechi la Ufundi 8 pamoja na viongozi 5.
Siku ya Jumatano na Alhamis jioni kikosi cha l Ahly kitafanya mazoezi katika Uwanja wa IST uliopoa Upanga, na Ijumaa jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo huo wa jumamosi.
Viingilio vya mchezo huo ni:
VIP A Tshs 35,000/=
VIP B & C Tshs 25,000/=
Orange Tshs 13,000/=
Blue & Green Tshs 7,000/=
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa katika Vituo Vifuatavyo:
Makao Makuu - Young Africans Sports Club - Twiga/Jangwani
Benjamin Mkapa High School - Uhuru
Kidongo Chekundu - Mnazi Mmoja
Buguruni - Oil Com
Dar Live - Mbagala
Uwanja wa Uhuru - Taifa Road
Steers - Samora Avenue
Oil Com - Ubungo
Mwenge Stand
Mbezi Mwisho - Stand



