You are here: Home NEWS Local News YANGA KUIVAA RUVU SHOOTING KESHO

YANGA KUIVAA RUVU SHOOTING KESHO

E-mail Print PDF

VIEWED 2524 TIMES

Young Africans kesho itashuka dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kupambana na timu ya maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara 2013/2014, huku mshambuliaji Emmanuel Okwi akitarajiwa kuonekana uwanjani kwa mara ya kwanza kwenye mikikimikiki ya VPL.

Kikosi cha Young Africans kilichoweka kambi mjini Bagamoyo kujiandaa na mchezo huo kimefanya mazoezi mepesi ya mwisho leo asubuhi kujiandaa na mchezo huo ambapo habari njema ni kwamba hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi kuelekea kwenye mpambano huo.

Kocha Mkuu Hans Van der Pluijm akiongea na mtandao rasmi wa klabu amesema vijana wake wote wapo fit, na morali ya wachezaji wote kwa ujumla ni nzuri hali kadhalika nidhamu ni bado ya hali juu na wachezaji wote wakiwa na umoja na upendo.

Kwa kweli vijana wangu wananipa imani kubwa sana kuelekea kwenye michezo inayofuata, wanajituma kila mchezaji ana hamu ya kuonyesha uwezo wake dimbani naamini kufikia siku ya mchezo watakaoamka salama ndio watakaovaa jezi kuanza katika mechi hiyo.

Siijui vizuri timu ya Ruvu Shooting lakini kwa kuwa kocha wangu msaidizi Charles Mkwasa alikuwa akiifundisha kwa muda mrefu naamini anawajua vizuri hivyo tutatumia mapungufu yao kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huo, malengo yetu ni kutetea Ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo alisema "Hans".

Wakati huo huo Kocha Msaidizi wa Young Africans Charles Mkwas anatarajiwa kuwasili leo usiku akitokea nchini Misri alipokwenda kushuhudia mchezo wa Super Cup kati ya Mabingwa wa Klabu Bingwa barani Afrika Al Alhy walipoichapa timu ya CS Sfaxien ya Tunisia Mabingwa wa Kombe la Washindi barani Afrika kwa mabao 3-2.

 

Last Updated ( Friday, 21 February 2014 13:21 )  

  • FACEBOOK

  • TWITTER