You are here: Home NEWS Local News YANGA KUWAFUATA WACOMORO KESHO

YANGA KUWAFUATA WACOMORO KESHO

E-mail Print PDF

VIEWED 2348 TIMES

Young Africans Sports Club wawakilishi wa Tanzania bara kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kesho watakwea pipa saa 6 kamili mchana kuelekea Visiwa vya Comoro tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Komorozine de Domoni utakaofanyika siku ya jumamosi katika Uwanja wa stade International Said Mohamed Cheik Mitsamiouli.

Kikosi cha mholanzi Hans Van der Pluijm kimekua kikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika Uwanja wa Karume makao makuu ya TFF kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa marudiano ambao ni muhimu kwa Young Africans kuendelea kufanya vizuri na kuweza kusonga hatua inayofuata.

Young Africans inatarajiwa kuondoka na shirika la ndege la Precision majira ya saa 6 kamili mchana na kuwasili Visiwa vya Comoro majira ya saa 8 mchana ambapo kikosi kitaelekea hotelini kupumzika kabla ya jioni kufanya mazoezi mepesi.

Katika mchezo wa awali uliochezwa mwishoni mwa wiki Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Komorozine mabao yaliyowekwa wavuni na Mrisho Ngasa (3), Didier Kavumbagu (2), Nadir Haroub (1) na Hamis Kiiza (1).

Msafara unatarajia kuwa na watu 30 wakiwemo wachezaji 19 Benchi la Ufundi saba (7) pamoja na viongozi wanne (4)

Magoikipa ni: Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"

Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani na Rajab Zahir

Viungo: Athuman Idd "Chuji", Frank Domayo "Chumvi", Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga na Hamis Thabit

Washambuliaji: Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Saimon Msuva na Mrisho Ngasa

 

Benchi la Ufundi:

Kocha Mkuu - Hans Van der Pluijm

Kocha Msaidizi - Charles Mkwasa

Kocha wa Makipa - Juma Pondamali

Daktari wa Timu - Dr Suphian Juma

Meneja - Hafidh Saleh

Mtunza Vifaa - Mahmoud Omar "Mpogolo"

Mchua Misuli - Jacob Onyango

Viongozi

Aaron Nyanda - Kamati ya Utendaji

Baraka Kizuguto - Afisa Habari

Mohamed Bhinda - Kamati ya Utendaji

Ramadhan Nassib - Mkuu wa Msafara kutoka TFF

Last Updated ( Wednesday, 12 February 2014 10:52 )  

  • FACEBOOK

  • TWITTER