You are here: Home NEWS Local News CAF ORANGE CL: YANGA VS KOMORIZNE KESHO

CAF ORANGE CL: YANGA VS KOMORIZNE KESHO

E-mail Print PDF

VIEWED 2929 TIMES

Wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika timu ya Young Africans kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya Komorozine de Domoni kutoka Visiwa vya Comoro kwenye mchezo wa awali wa mashindano hayo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans ambayo imeweka kambi mjini Bagamoyo kujiandaa na mchezo huo, imekua ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku kujiandaa na mchezo huo ambao watoto wa Jangwani wamedhamiria kuibuka na ushindi.

Komorozine de Domoni ambao ndio wawakilishi wa Visiwa hivyo tayari walishawasili tangu majuzi na jana waliweza kufanya mazoezi katika Uwanja wa Karume asubuhi na jioni na leo jioni wakitarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja waTaifa ambao utatumika kwa mchezo huo wa kesho.

Kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Pluijm amesema maandalizi ya mchezo wa kesho kwa kikosi chake yamekaliika, vijana wote wako fit, kiakili na morali ni ya hali ya juu hivyo naamini tutaibuka na ushindi katika mchezo huo.

Nimekua na timu kwa takribani wiki nne sasa tangu niungane na wachezaji nchini Uturuki, maendeleo ni mazuri mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City tumeyafanyia kazi na kwa sasa kikosi kimezidi kuimarika.

Mchezo wa kesho unatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki, wapenzi, washabiki na wanachama wanaombwa kujitokeza kwa wingi kesho Uwanja wa Taifa kuja kuwashangilia vijana wao watakapokuwa wanaipeprusha bendera ya Taifa.

Last Updated ( Friday, 07 February 2014 10:45 )  

  • FACEBOOK

  • TWITTER